Muandishi: Hii ina maana mpaka sasa upo na Bongo records? na kama ni hivyo ushafanya kazi gani nyingine na label hii?
Mike Tee: kwasasa sipo tena Bongo Recoeds kwasasa nafanya kazi sana kwenye studio yangu mwenyewe iitwayo MyKey Records ipo nyumbani tu ndugu yangu nakesha nikifanya track zangu kama kwenye album yangu hii mpya ya NIACHENI nimefanya track kama tunakuja,kabla ya,sikiliza ni ambazo nimekesha nazo mwenyewe na ukisikia utaona ni tofauti production na production nyingine za hapa bongo.
MUANDISHI: washabiki wako wategemee lini hiyo album kuwa sokoni?
Mike Tee: tarehe 29 aapril ndio nilipanga me na msambazaji wangu FKW kuwa album yangu itakuwa sokoni pia natoa video nyingine kali ili isaidie kusukuma mauzo ya album hiyo nimeifanya na AY na SNARE wote toka ECT inaitwa NISINGENG'ARA chini ya kampuni ya WANANCHI VIDEO PRODUCTION.Pia hivi sasa najiandaa kufyatua kitu kingine kwa kushirikiana na dada yangu, Anna Mwakatundu (Miss Mzumbe mwaka 2002)
MUANDISHI: mpaka sasa una albam ngapi? na umepata mafanikio gani kwenye muziki mwisho unaushauri gani kwa wasanii wenzako hasa ukitilia maanani kuwa fani hii sasa imepata washabiki na kukubalika katika jamii?
Mike Tee: Mpaka sasa nna album tatu SINTOBADILIKA,JE UTANIPENDA? NA NIACHEN,Mwezi December nategemea kutoa album nyingine iitwayo BADO TU? siwezi kusema muziki umenipa mafanikio sana kwasababu najulikana sana kuliko bank statment inavyosoma mzee Bongo sasa ni umaarufu kuliko pesa, wasanii nawashauri waende shule kwasababu muziki bado sio ajira ni kitu cha kupita so tusilewe na umaarufu tuangalie waliotangulia wapo wapi.