MUANDISHI: ni wasanii gani unaowakubali ukianzia hapa nyumbani?
Mike Tee: nikianzia nyumbani ni Lady Jay Dee kwasababu kazi yake nadhani wengi wanaijua na mimi alikuwa ni mtu kwanza kufanya nae kazi na akanitoa na mambo aliyoyafanya kuwakilisha Tanzania kule kwa Tabu Mbeki mmesikia kwa nje ya nchi ni Eminem na Dre.
MUANDISHI: Nini matarajio yako baada ya kutoa album yako mpya ya hii NIACHENI?
Mike Tee: Kaka kutokana na majukumu ambayo yananikabili baada ya kutoa album kwanza nitaangali watu watasemaje kuhusu production zangu binafsi kwasababu nataka sana kuwa mtayarishaji wa muziki hapa nchini so napenda sana kuwa kama Dre jinsi alivyo nami nataka niwe hivyo.
MUANDISHI:JE kuna lolote unaweza ukawa nalo la nyongeza kwa mashabiki wako?.
Mike Tee:mashabiki nawasihi wasikate tamaa kunishauri kunikosoa nnapokosea au kupatia kunisifia,ila nategemea tena kutoa album ya video ambayo itaonyesha maisha yangu halisi itakuwa na story toka home mpaka kwenye fani then itakuwa na trak kumi za video kama na nyaluland ikiwa ndani,thanx for your time.
Basi hayo ndio machache kama sio mengi kuhusu Mike Tee wasanii kazi kwenu challenge hiyo toka kwa Mnyalu.
Je mnajiamini kiasi cha kutoa single saba ?halafu msiweke kwenye album ?ha! ha! ha! ha! 'Samaki wengi maji machache' je mtavuka?