LYRICS: JE UTANIPENDA?

TRACKS.
1.Sintobadilika Ft. Q-Chillah,

PRODUCED By MJ Records CHORUS HATA KAMA MNYALU NASIKIKA KWENYE CD/ HATA KAMA MNYALU NAONEKANA KWENYE TV/ HATA KAMA MNYALU NAONEKANA KWENYE TV/ HATA KAMA MNYALU NATOKEA GAZETINI IIII NAWASIHI SINTOBADILIKA VERSE wanamalenga wanalia machozi ya kuhofia/ wakidai muda wa mabadiliko umewadia/ mnyalu kutengana na nduguze kisa mali/ kujiona fahari apitapo kila mahali/ baba mama maswali mpenzi nae maswali/ jamii ya kinyalu yote imejaa maswali/ je, nikipata umaarufu ntakuwa kama awali/ ama ntawaona wao tena kwangu si mali/ manatoa maneno na mifano mingi ya awali/ ya watu waliopita ambao walikuwa mashuri/ imebaki historia may b kwangu itajirudia/ lisemwalo lipo kama halipo linajongea/ eti ndugu jamaa marafiki ntawadisi/ salamu kwa washikaji zangu itakuwa basi/ heshima kwa wazazi itashuka c kama zamani/ hata asali wangu wa moyo sintomthamini/ kisa nimebadili mfumo wangu wa maisha/ kujimix na watoto wa uswazi hadhi inashuka/ milupo kila day kama nguo ntabadilisha/ ponda mali kufa kwaja msemo hautoniisha/ kifua ntatunisha miondoko ntabalisha/ mavazi marafiki usafiri ntabadilisha/ kuonyesha msisitizo lugha nayo ita badilika/ badala ya kamwene kwangu hi ni whats up/ hey yo jay CHORUS HATA KAMA MNYALU NASIKIKA KWENYE CD/ HATA KAMA MNYALU NAONEKANA KWENYE TV/ HATA KAMA MNYALU NAONEKANA KWENYE TV/ HATA KAMA NATOKEA GAZETINI IIII NAWASIHI SINTOBADILIKA VERSE2 Mengine kibao yamezuka kwangu chumbani/ honey anadai nimechange siko kama zamani/ saa saba mchana kwenye line sipatikani/ niko busy kwa mj au busy na fani/ fani mikwanja na madini shingoni/ fani inaleta pamba misosi hapo mezani/ lakini unadai nichague fani na penzi/ bila fani honey mnyalu siwezi kumiliki benz/ unaniona mshenzi nisiye na akili kichwani/ ambae nataka penzi lipotelee hewani/ unata nini nifanye unione kama zamani/ ama niendelee kuongea kinyalu hadharani/ nikimwona mj nimwambie kamwene munogage/ we unataka wanga wa disala watuloge/ ntafanya utakacho ili penzi letu linoge/ mikufu sarafu umaarufu isivuruge/ ahadi ya pete lazima itakamilika/ uidhani nimesheheni tamthiria za kusadikika/ kila kitu ni kama kila kitu ni kama/ tuliza ball honey sintobadilika hey yo jay/ CHORUS HATA KAMA MNYALU NASIKIKA KWENYE CD/ HATA KAMA MNYALU NAONEKANA KWENYE TV/ HATA KAMA MNYALU NAONEKANA KWENYE TV/ HATA KAMA NATOKEA GAZETINI IIII NAWASIHI SINTOBADILIKA BRIDGE hata kama naheat dar es saalama wanyalu siwezi uwamwaga/ hata kama nina demu wa kiasia wa kibongo siwezi kummwaga/ mshike mwenzio mkono mwambie mnyalu hatobadilika/ mnong'oneze mwenzio sikio mwambie mnyalu sintobadilika/ tuimbe wote sintobalika/ tuimbe sote sintobadilika/ tuimbe wote sintobadilika aaaaa aaa nana nana CHORUS HATA KAMA MNYALU NASIKIKA KWENYE CD/ HATA KAMA MNYALU NAONEKANA KWENYE TV/ HATA KAMA MNYALU NAONEKANA KWENYE TV/ HATA KAMA NATOKEA GAZETINI IIII NAWASIHI SINTOBADILIKA,

2.NAMPENDA NANI Feat JUMA NATURE PRODUCED By pFUNk (BONGO RECORDS),

CHORUS: nakupendaaa na sifa nakupa [mnyakwibata],usiyafuate ya wale wasiopenda maendeleo yako mpenzi wangu x2/ nampenda penda [naaani] msichana mmoja [naani],mweupe kidogo[naaani],nampenda nampenda/nyuma kajaza[naani],kifuani---[naani],anakwenda kwa pozi naani,nampenda nampenda VERSE: Nampenda dem mmoja awe mtanzania/awe na sifa za kweli niweze jivunia/nijue wapi kazaliwa wapi katokea/ndugu jamaa wazazi nipate waelezea/uzuri wa sura yake uendane na tabia/apendwe na watu c makumi bali mamia/dada zangu wazazi wasije kumchukia/waseme mbona cc awali tulikuambia/ntampenda dem mwenyewe awe mweusi kidogo/hata kama mweupe isiwe kwa mkorogo/awe mnyisanzu mnyakyu mnyalu c mgogo/hapo ntapata raha kachaa c kidogo/niwe kwake moyoni asiwe kwangu mfukoni/eti umaarufu na madini yangu shingoni/dem yamdatishe anase kwangu mtegoni/ntapochalala dem aingie mitini/sijui nani mkweli sijui nani nimwamini/ila namwomba mungu roho tu ya imani/nimpate mmoja mpenzi tu nimwamini/nimvike pete ndoa kitu cha thamani/utajiri umaskini ndani ya penzi ni matokeo/kila mmoja kati yetu atambue jambo hilo/isije siku za usoni ikaleta kimeo/lakini nakuamini huwezi kuniacha mwenzio/utabaki wangu nami ntakuwa wako/kile kilicho changu mpenzi hicho ni chako/bega kwa bega nami niko nyuma yako/mike tee na nature haki ya mungu hatutoficha/ CHORUS nakupendaaa na sifa nakupa [mnyakwibata],usiyafuate ya wale wasiopenda maendeleo yako mpenzi wangu x2/ nampenda penda [naaani] msichana mmoja [naani],mweupe kidogo[naaani],nampenda nampenda/nyuma kajaza[naani],kifuani---[naani],anakwenda kwa pozi naani,nampenda nampenda hewala bwana wacha me niseme sana/hata nikificha kwangu haitoleta maana/ni kheli niwe mkweli muwazi anijue vizuri/ili akipata nyeti za uzushi awajibu kiburi/nafaham unafaham binadam sote dhaifu vizingiti ni vingi mpaka me nikuite wife/imani uvumilivu pia uaminifu/vyote kwa pamoja vyahitajika maradufu/mikufu sarafu isiwe kipimo cha mapenzi/kunikubali mnyalu nidrive bima au benzi/hizo ni fikra potofu tena tu za kishenzi/naahidi kwa kila khali mimi nitakuenzi/nataka uwe simple wabaki na mshangao/wale unaofanana na usiofanana nao/nikizuka nawe msichoke wote wabaki ooh/dem msomi ngeli no anaongea kikwao/mfano kukataa anasema ndeema/kila sehem nikimgusa anaheeema/kusema toka hapa anasema hege ipa/ngoma ikikataa anasema imenyopa/asante ntakufundisha wewe kusema ndaga/hivyo ndivyo mapenzi ya kinyalu yanavyokwendaga/tuombe uzima vyote me ntatimiza/ukiniona mike tee satisfaction guarantee CHORUS nakupendaaa na sifa nakupa [mnyakwibata],usiyafuate ya wale wasiopenda maendeleo yako mpenzi wangu x2/ nampenda penda [naaani] msichana mmoja [naani],mweupe kidogo[naaani],nampenda nampenda/nyuma kajaza[naani],kifuani---[naani],anakwenda kwa pozi naani,nampenda nampenda nampenda penda [naaani] msichana mmoja [naani],mweupe kidogo[naaani],nampenda nampenda/nyuma kajaza[naani],kifuani---[naani],anakwenda kwa pozi naani,nampenda nampenda CHORUS nakupendaaa na sifa nakupa [mnyakwibata],usiyafuate ya wale wasiopenda maendeleo yako mpenzi wangu x2/ nampenda penda [naaani] msichana mmoja [naani],mweupe kidogo[naaani],nampenda nampenda/nyuma kajaza[naani],kifuani---[naani],anakwenda kwa pozi naani,nampenda nampenda [x3),

3.; NIBEEP baby Feat MAD ICE N MISSIE ANNIE PRODUCED by MJ RECORDS,

chorus nibeep baby - nimekumiss sana honey nibeep baby - mi nataka kwenda hewani nibeep baby - nimekumiss sana honey hivi ni nani mnyalu atanifariji verse 1 ni siku kibao sijakutia machoni tangu siku tumeachana a-town ulinipromise utakwenda hewani siku ambayo utafika kwenu nyumbani ulisema huna simu ya mkononi nikuchore namba yangu kiganjani utapofika kwenu huko unyaluni upate nipigia hata kibandani sasa naona kimya kimezidi hakuna beep hakuna sms hivi ni nani mnyalu atanifariji embu nibeep embu nibeeeeep chorus nibeep baby - nimekumiss sana honey nibeep baby - mi nataka kwenda hewani nibeep baby - nimekumiss sana honey hivi ni nani mnyalu atanifariji verse 2 bonyeza namba zangu mpenzi nenda hewani japo unibeep mimi niende hewani nijisikie kama upo pembeni niweze ipata faraja moyoni siku masaaa dakika zinapita hata ujumbe wa maneno sijapata jambo gani baya limekukuta moyo wangu unaanza pitapita maana naona kimya kimezidi hakuna beep hakuna sms hivi ni nani mnyalu atanifariji embu nibeep embu nibeeeeep chorus nibeep baby - nimekumiss sana honey nibeep baby - mi nataka kwenda hewani nibeep baby - nimekumiss sana honey hivi ni nani mnyalu atanifariji verse-missie annie ningekubeep honey ningekwenda hewani, lakini dingi na mother wamekaa sebuleni, dingi amekaa pembeni kwenye ttcl, mother amepoa pembeni anacheki video, after all simu yangu imekwisha dola, ya mezani nikigusa kwa dingi msala, ya bro kimeo ukibeep yakata power, ya sister hawa anadai imeuwawa, BRIDGE namba unayobeep is not beepable jaribu baadae x4 chorus nibeep baby - nimekumiss sana honey nibeep baby - mi nataka kwenda hewani nibeep baby - nimekumiss sana honey hivi ni nani mnyalu atanifariji,

4.Hodi,

5.N I A C H E N I ft Banana Zorro,

Producers ; Mj records,Bizzieman,Rajab Marijan,

Written by ; Mike Tee,

Chorus; niacheni mie eeh nikeshe nae huyu kimwana mbali mimi nimetoka nae tukiachana sie furaha iwe kwenu nyie moyoni mwangu mimi nizidi kupata tabu VERSE kwenye tambarare milima mabonde si tulishuka/ baadhi ya mizigo yangu mizito ulijitwika/ kwenye dhiki na raha hukuniacha/ ndicho kitu kimoja ambacho mimi nafarijika/ wanok nok vinabo wanavuka mipaka/ maneno wanayopaka mitaani mimi nachoka/ hawafahamu ni wapi tulipotoka/ na wapi ahadi yetu tumeweka kufika/ nilishasema kwake sintobadilika/ na hii mara ya tatu narudia tena kunena/ ndani ya nafsi popote nilipo yupo/ sintoweza saliti kisa nilipo haupo/ maneno kibao wengi wameongea/ wengine washikaji hasilani nawamezea/ madai yao mbali ulitupilia/ ulijua wapumbavu chokochoko wamezoea/ binadamu nna imani sote dhaifu/ vizingiti ni vingi pale unaposaka wife/ kama me jinsi nnavyokwenda/ nna imani ntasimama imara nami ntashinda/ Chorus; niacheni mie eeh nikeshe nae huyu kimwana mbali mimi nimetoka nae tukiachana sie furaha iwe kwenu nyie moyoni mwangu mimi nizidi kupata tabu VERSE 2 ni nini napenda kwake hiyo ni siri yangu/ kama chaguo langu ni siri ya mola wangu/ iweje leo hii unipangie na maisha yangu/ kimwana anaefaa awe mama watoto wangu/ kama kumpenda nimempenda mimi mwenyewe/ sababu kibao ninazozijua mwenyewe/ katiba inasema binadam sote sawa/ lakini kimawazo na utashi hatuko sawa/ kwenye mapenzi sisi tunatofautiana sana/ kila mmoja anavutiwa kivyake mbele ya msichana/ kitu gani utasema kwangu mi nikuelewe/ niachane nae au kuishi utakavyo wewe/ nimeridhika nae nimependa jinsi alivyo/ uzuri sura yake tabia alizonazo/ kusema nampenda hadhari me sintochoka/ mpakakwenye futi sita chini ntaposhuka/ eti ananipenda kisa mi ni supastaa/ hawajui ni toka tanangozi si tunakaa/ eti amezuzuka na madini shingoni/ hawajui mapendi yeu tumeanza kwenye khali duni/ Chorus; niacheni mie eeh nikeshe nae huyu kimwana mbali mimi nimetoka nae tukiachana sie furaha iwe kwenu nyie moyoni mwangu mimi nizidi kupata tabu bridge kama kumpenda niliamua mwenyewe vp kumuacha unipangie wewe kama kunipenda aliamua mwenyewe hata kuniacha ataamua yeye yaani nampenda kumuacha sintaweza jinsi nnavyompenda sintoweza kumtelekeza binti kaniweza na mi nimemuweza tunapendana hatutotenganaaa Chorus; niacheni mie eeh nikeshe nae huyu kimwana mbali mimi nimetoka nae tukiachana sie furaha iwe kwenu nyie moyoni mwangu mimi nizidi kupata tabu,

6.kama feat JAY MOE,

PRODUCED By PfUNK (BONGO Records),

mawazo kichwani sawa na tamthilia ya kusadikika/ kuwa na magari majumba yasiyohesabika/ niishi maisha iringa kama niko amerika/ sababu nna mkwanja ningemuoa mtoto maraika/ ningekuwa mrefu kwenye mkapu ni patashika/ ningewapa madunk yale ya kukata na shoka/ ningechora tatoo kichwani nywele ningesuka/ kuonyesha msisitizo kiswahili kisingesikika/ ningependa kuongea lugha ya asili nilikotokea/ kangi jope ughonile si unanyaka/ mistari yangu verse kinyakyusa ningeiandika/ na kufanya lugha yangu kisanii kutambulika/ maisha yangu yangekuwa hadithi kihesa mpaka isoka/ mpenzi wangu angepata achotaka kile anachotaka/ fedha ingeonga sauti yangu ingesikika/ shikamooo mzee ningepata kwa kila rika/ wapambe ningekuwa nao wasiohesabika/ hata niongee upumbavu makofi yangesikika/ ningefanya uharifu polisi nao wasingenishika/ kunako mahakama mshiko wangu ungetumika/ vyombo vya dola sheria za nchi ningezishika/ nembo ya taifa bongo records ingetumika/ watoto wadogo lazima mic wajue kushika/ lakini yote hii ni kama kama chorus; (kama) mike tee ningekuwa staa/ (kama) ningekuwa na mkwanja kachaa (kama)ningekuwa me mrefu nna mkwanja kachaa iringa town ingekuwa balaa kama ninge kama ningekuwa mimi staa/ hakika jina kila mtaa lingezagaa/ anzia ngazi ya shina tawi mpaka mkoa/ vibanda vya mamc katuni vyote ningebomoa/ ningepewa sifa nyingi za marehem/ na kuonekana kama nusu mtu nusu mzim/ madem wangesema mike tee we handsome hata kama uso wangu una makovu kila sehem/ ningenunua benz sita zote rangi ya bluu/ mkata majani wangu asingetembea kwa mguu/ masela akitaka jiti namkatia bluu/ na kumuonyesha mambo yangu ni safi usawa huu/ kwakuwa nna mkwanja hata muumba angesahahaulika/ huku kuingia peponi ningekuwa nna uhakika/ kwa kujipa moyo mbona natoa nyingi sadaka/ jina langu siku ya mwisho halintosahaulika/ kwa pumba kachaa ahaa ntakuwa nnasifika/ kinyalu mdomoni hakika hakitonitoka/ kama kutosa mi ntasema kudaga/ na ntajenga kilabu kikubwa cha pombe dabaga/ ntapeleka muswada bungeni ulanzi uitwe lager/ uuzwe supermarket za bongo hata canada/ watu wapate mshiko wanyalu waache kidada/ music awrd za mtoni zifanyike dabaga/ ntajenga trade center ya kimataifa tanangozi/ mabitozi wa kinyalu wasiosoma watakwenda kozi/ ili wapate ujuzi waache ubabaishaji lakini yote hii ni kama kama chorus; (kama) mike tee ningekuwa staa/ (kama) ningekuwa na mkwanja kachaa (kama)ningekuwa me mrefu nna mkwanja kachaa iringa town ingekuwa balaa chorus; (kama) mike tee ningekuwa staa/ (kama) ningekuwa na mkwanja kachaa (kama)ningekuwa me mrefu nna mkwanja kachaa iringa town ingekuwa balaa chorus; (kama) x 6 chorus; (kama) mike tee ningekuwa staa/ (kama) ningekuwa na mkwanja kachaa (kama)ningekuwa me mrefu nna mkwanja kachaa iringa town ingekuwa balaa chorus; (kama) mike tee ningekuwa staa/ (kama) ningekuwa na mkwanja kachaa (kama)ningekuwa me mrefu nna mkwanja kachaa iringa town ingekuwa balaa,

7.Cheza kwa Usalama,

8.Hellow

© 2005,MyKeY Records & MNYALU INC. All rigths reserved.

Back Home
album info
hit singles
interviews
sing along lyrics
updates

NEW ALBUM IS OUT
"JE UTANIPENDA" click here for more

HOME | ALBUMS | SINGLES | INTERVIEW | LYRICS | NEWS | CONTACTS |

© Mike Tee,2004. All rights reserved. Developed by KiDesigns

Hosted by www.Geocities.ws

1