INTERVIEWS WITH OUR REPORTER CONTINUES

bila kupoteza wakati maana najua kwa wakoloni time ni mshiko au vipi?inabidi sisi tuende kimtindo huo au sio mwanangu? ha ha ha!! hebu tumwagie historia yako kwa ufupi

Mike Tee: Kwa kifupi mimi nilizaliwa huko Iringa mwaka 1978 kwenye familia yenye watoto sita mimi nikiwa wa kwanza, na nilipata elimu yangu ya msingi katika shule ya Msingi Ilala na masomo ya awali ya sekondari katika shule ya sekondari ya Lugalo hukohuko Iringa,na unajua bwana mambo hayo ya rap nilianza toka nikiwa sekondari,na kwa kweli mtu aliyenipa hamasa au kishawishi cha fani hii alikuwa jamaa mmoja wapo katika kundi lililovuma sana kipindi hicho hapa nchini la 'Weusi Wagumu Asilia', WWA, anayejulikana kama Ntwa Mwandemani Kaisi (Tony Nice) ambaye kipindi hicho alikuja kwa masomo yake ya juu pale Mkwawa sekondari mwaka 1995.


MUANDISHI : Baada ya hapo mliunda kundi au mlikuwa mnaimba kwa kujifurahisha tu?

Mike Tee: Yap mzee,kipindi hiko ndio nilikuwa nimemaliza masomo ya awali ya sekondari,na tulikuwa tayari tumeanzisha kundi letu lililojulikana kama TDC(The Dangerous Cruise)nikiwa na mwenzangu Crazy Dog hiyo ilikuwa ni mwaka 1996,na mwaka mmoja baadaye tukamshirikisha dada yangu aitwaye Anna Mwakatundu tulitoa album yenye truck 8 iitwayo 'Hii ni Afrika' ambayo ilibeba nyimbo kama ,Hivi kweli tutafika,Sisi Vijana na Gumzo.Lakini kutokana na kubanwa na masomo ikabidi tena niende darasani katikati ya mwaka huo,ambapo nilienda Mbeya katika Seminary ya Manow Lutheran.Baada ya kitabu mwaka 2001 nikiwa na washikaji zangu wengine tuliokutana nao Mbeya kama Adili,Ras Raja na Seif tulitoa kitu chetu kiitwacho tamati kilichotamba kidogo.Mwaka huohuo nilipata nafasi katika Chuo cha Taifa cha Biashara CBE, ambapo nipo mpaka sasa nikichukua Diploma ya Biashara, na hapo nikaamua kuingia Studio na kurekodi single iliyokwenda kwa jina la Nyaluland nikiwa nimemshirikisha Lady Jay Dee chini lebo ya Bongo Records.

PREVIOUS | CONTINUES

Back Home
album info
hit singles
interviews
sing along lyrics
updates

IN STORES 29TH APRIL 05
"JE UTANIPENDA AND NIACHENI ALBUM" click here for more

HOME | ALBUMS | SINGLES | INTERVIEW | LYRICS | NEWS | CONTACTS |

© Mike Tee,2005. All rights reserved. Developed by KiDesigns

Hosted by www.Geocities.ws

1