Global Village (Kijiji Cha Tufe Lenye Sura Ya Dunia)
Global Village ni chama cha utamaduni kinachowaakilisha watu wa nchi tofauti. Chama hiki kimeundwa ili kiweze kuwafaidi wenye chama kuelewana na kushauriana kwa mawazo tofauti yanayo husu nchi mbali mbali. Marafiki wachache kutoka uko tofauti humu Tampere waliwasiliana kiangazi cha mwaka 2000 kwa nia ya kuanzisha chama ambacho kitacho akilisha mahitaji yao. Marafiki hawa walitoka katika eneo mbali mbali za ulimwengu huu. Nia yao ilikua ya kushirikiana, kuwapokea na kuwakaribisha wageni humu Tampere kwa ajili ya, kuwaelimisha namna za kuishi kwa utamaduni wa Kifini.
Global Village ikazaliwa. Njia za kutimiza mahitaji haya zikafunguliwa. Wafusi wa chama hiki wamefanikiwa na elimu katika viwango vingi. Elimu na ujuzi huu ndio kianzisho cha kuwaelimisha wageni wanaowasili, na wenye chama ambao wanaohitaji kuongeza maarifa yao. Mwaka uliopita Global Village iliweza na inaendelea kuyatimiza matakwa haya:

*Kuratibisha kila mwezi mambo ya utamaduni tofauti na kuwafundisha wajiji wa Tampere kuhusi utamaduni huu.
*Kuwaelimisha kwa kujitolea kila wiki, wanafunzi ambao wanao hitaji elimu katika mafunzo mbali mbali, hasa hasa wageni.
*Kuunganisha vyama vya kigeni vya urafiki kwenye nia ya kushirikiana ili tuweze kusaisiana vile tuwezavyo.
*Kuunganisha vyama vya hiari vya kigeni kwa kusaidiana ili tuweze kutimiza maisha yetu kwenye mambo/mawazo yenye muhimu/faida hata wakati tusipokuwa na kazi.
*Kuunganisha kwenye kitabu, ama barua za umeme, habari za mji wa Tampere na nchi ya Finland.
*Kuanzisha ushirikiano unaofaa kati ya wanaowasili na wale ambao wamesha ishi huku kwa mda mrefu.

Mawazo ya wakati ujao ni ya kufungua mkahawa, eneo la utendaji na kuandika gazeti la wageni. Gazeti hii itawajulisha wasomaji masharti yao na jinsi ya maisha mjini Tampere. Global Village ni chama kichanga ambacho kinahitaji ushiriki na mawaidha yako. Kwenye kujitolea, unaweza kuwasaidia wenzako na vile vile, kujisaidia wewe mwenyewe. Simu za waakilishaji zafwatilia:
Angie Pohja -0400-777-530
David Landy -0442-933-244

Ama kwenye barua ya umeme
www.geocities.com/gv_tampere
Back To Main Page
Hosted by www.Geocities.ws

1